Tunu Kuu
1. Weledi
Tunatekeleza majukumu yetu kwa kutoa huduma bora tukizingatia maadili na heshima kwa wateja wetu;
2. Uwezeshaji
Tunawajengea uwezo wafanyakazi wetu ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto ikiwamo kuwapa fursa za kufanya uamuzi wakati wanapotekeleza majukumu na kutimiza wajibu wao;
3. Ubunifu
Tunazingatia ubunifu katika kushughulikia masuala ya kiudhibiti sanjari na mabadiliko ya teknolojia duniani;
4. Uadilifu
Tunatekeleza kazi zetu kwa kuzingatia maadili, uthabiti na uaminifu wa hali ya juu;
5. Utendaji wa Pamoja
Tunaamini katika utendaji kazi wa pamoja ili kutatua matatizo na kutambua kwamba mawasiliano imara ni muhimu katika kujenga mazingira ya ushirikiano;
6. Uwajibikaji
Tunawajibika kikamilifu na kuchukua dhamana tunapotoa huduma; na
7. Usawa
Tunaamini katika kutoa fursa na haki sawa kwa wadau wetu wa ndani na nje.
Malengo
Mamlaka imeandaa Malengo mbalimbali ili kufikia maono yake katika kukabiliana na mambo muhimu kama yalivyobainishwa katika uchambuzi wa hali halisi ya kisekta. Malengo hayo ni:-
- Kukuza miundombinu na huduma za mawasiliano ya kielektroni na posta yenye usalama, ufanisi na imara;
- Kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya kielektroni na posta zenye ubora na unafuu;
- Kuimarisha ubunifu wa huduma zinazodhibitiwa, uandaaji wa maudhui ya ndani na ujanibishaji;
- Kuimarisha ufanisi wa huduma zinazodhibitiwa na kuwalinda wadau; na
- Kuimarisha uwezo wa taasisi.